Masharti na Vigezo vya Test Zali

Kwa kushiriki katika promosheni ya Test Zali, mteja anakubali masharti na vigezo vifuatavyo:

Tafadhali soma kwa makini kabla ya kujiunga au kuendelea kutumia huduma ya Test Zali.
1

Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa kulipia kabla wa Yas pekee.

2

Washiriki lazima wawe na umri wa miaka kumi na nane (18) au zaidi ili kushiriki.

3

Promosheni hii ni kwa wakazi wa Tanzania pekee.

4

Wafanyakazi wa Yas na Green Telecom pamoja na familia zao za karibu hawaruhusiwi kushiriki katika promosheni hii.

5

Namba ya mteja lazima iwe imesajiliwa kwa utambulisho wa alama za kibayometriki ili kutumia huduma hii.

6

Zawadi za promosheni hii haziwezi kubadilishwa, kuhamishwa au kupewa mtu mwingine yeyote.

7

Kwa kushiriki katika huduma hii, mteja anatoa ridhaa moja kwa moja kupokea ujumbe wa matangazo ya huduma wakati wowote atakapokuwa ndani ya huduma.

8

Majina ya washindi yatatangazwa kupitia vyombo maalum vya habari za kielektroniki, tovuti za Yas na kuchapishwa kwenye magazeti yaliyochaguliwa.

9

Kwa kushiriki katika promosheni hii, mteja anathibitisha kuwa amesoma, kuelewa na kukubaliana na masharti na vigezo vya promosheni hii.

10

Yas ina haki ya kubadilisha masharti na vigezo vya promosheni hii wakati wowote kwa kutoa taarifa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT - The Gaming Board of Tanzania).

11

Washindi wote watajulishwa kupitia simu kwa namba 100. Mteja ambaye hatapatikana au hatapokea simu mara tatu (3) hatakuwa na haki ya kudai zawadi na malalamiko yoyote yatakuwa batili.

12

Wateja wote wanatakiwa kusoma na kuelewa masharti yote kabla ya kujiunga na huduma; matatizo yatokanayo na kutoelewa, kutofuata na kutii masharti na vigezo yatapuuziwa.

13

Baada ya kujiunga na huduma, watumiaji wote watakatwa kiasi fulani kila siku ambacho kinawawezesha kubaki katika mchezo na kupewa nafasi baada ya makato hayo ili kujaribu bahati yao ya kuweza kushinda. Endapo nafasi hiyo haitatumika, haitarejeshwa wala kulipiwa fidia ya aina yoyote.

14

Neno lolote lisilo sahihi litakalotumwa kwenye namba 15306 litachukuliwa kama jaribio la kushiriki katika mchezo ili mtumiaji aweze kushinda zawadi, na gharama zitakatwa kulingana na kiwango kilichowekwa kwa ajili ya kushiriki kwenye mchezo husika.

15

Mshiriki yeyote aliyeshinda zawadi lakini hatapatikana au hatapokea simu mara tatu (3) atapoteza ushindi wake. Katika hali hiyo, droo mpya itafanyika kumpata mshindi mwingine.

16

Zawadi zote za promosheni ya TESTI ZALI zitatolewa kwa washindi katika ofisi za Yas walizoelekezwa wakati wa kupigiwa simu kupitia namba rasmi ya huduma kwa wateja (100) pekee na wala si namba yoyote. Malalamiko ya kuwa umeshinda bila kutaarifiwa kupitia namba 100 ni batili na wala hayatosikilizwa.

17

Majina ya washindi yatatangazwa kwenye vyombo maalum vya habari za kielektroniki na kuchapishwa kwenye magazeti kwa madhumuni ya promosheni.

18

Waendesha kampeni wanaweza kutumia majina fulani katika jumbe za kuhamasisha washiriki waendelee kucheza na kuangalia bahati zao za ushindi. Matumizi ya majina hayo hayamaanishi kuwa mtu huyo ameshinda kwani ushindi wowote unaweza kutangazwa kwa kupigiwa simu kwa kutumia namba 100 tu na si vinginevyo.

19

Zawadi za promosheni hii haziwezi kubadilishwa, kuhamishwa au kupewa mtu mwingine.

20

Mshindi atalazimika kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambulika kitaifa kabla ya kuthibitishwa rasmi kama mshindi.

21

Yas ina haki ya kubadilisha masharti na vigezo vya promosheni hii wakati wowote kwa kutoa taarifa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

22

Zawadi zote za fedha zitakatwa kodi ya asilimia 15 (15%) ya michezo ya kubahatisha kulingana na maelekezo ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania - GBT).

23

Yas ina haki ya kubadilisha masharti na vigezo vya promosheni hii wakati wowote kwa kutoa taarifa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Mwisho wa kusasishwa: Aprili 2026.